Recent Articles

Wednesday, March 26, 2014

KUELEKEA MIAKA MITATU YA BONGO MOVIE UNIT...

Wednesday, March 26, 2014 - by Unknown · - 0 Comments

Tar 28/3/2014 Bongo Movie Unit inatarajiwa kutimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa. Windhoek Draught wakiwa ndio wadhamini kwa siku yetu hiyo walituwezesha kupeleka mahitaji mbalimbali kwenye wodi ya kinamama na watoto ya hospitali ya Mwananyamala.Ikumbukwe kuwa kinamama na watoto ndio wateja wakubwa wa filamu zetu.

Angalia picha za yaliyojiri leo kwenye tukio hilo...wasanii wengi walijitokeza kufanikisha zoezi hilo...

Tuesday, January 14, 2014

PICHA TATU ZA YALIYOJIRI SAFARINI KUTOKEA ZANZIBAR........!

Tuesday, January 14, 2014 - by Unknown · - 0 Comments




Saturday, January 11, 2014

PICHA: UZINDUZI WA MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA MWANZA

Saturday, January 11, 2014 - by Unknown · - 0 Comments


Mashindano ya Maisha Plus / Mama Shujaa wa Chakula  yametambulishwa rasmi kwa wakazi wa jiji la Mwanza katika viwanja vya shule ya msingi Buhongwa.. 



Waandaaji wa mashindano hayo wakiambatana na Balozi wa kampeni ya Grow Jacob Stephen maarufu kama JB pamoja na Jack Monroe ambaye ni Mwanawavuti kutoka nchini Uingereza walifika viwanjani hapo na kulakiwa na umati wa watu waliokuja viwanjani hapo ili kufahamu zaidi kuhusu Maisha Plus / Mama Shujaa wa Chakula.

Angalia picha za matukio yaliyojiri.........

Jack Monroe na JB
"Kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu, tusikate tamaa", alisema JB.
Huyu ni Khadija Liganga kutoka shirika lisilo la kiserikali la Kivulini la jijini Mwanza. Khadija amefanya kazi nzuri sana kama mshereheshaji wa shughuli hizi.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika viwanja vya shule ya msingi Buhongwa.
Kikundi cha Ngoma na michezo ya nyoka wakitumbuiza katika uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula jijini Mwanza.
Eluka Kibona ambaye ni Meneja wa kampeni, ushawishi na utetezi kutoka Oxfam akizungumza katika hafla hizo.
Sharon Mariwa kutoka Oxfam akizungumza katika hafla hiyo
Teresa Yates, Mratibu wa kitengo cha Haki Jinsia kutoka Oxfam akizungumza katika hafla hizo.
Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwataka vijana kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kuchangamkia fomu za Maisha Plus.. Milioni 25 itatolewa kwa mshindi..
Baadhi ya wakina mama waliojitokeza kushiriki shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakipokea fomu kutoka kwa Balozi wa Grow JB.
Baadhi ya vijana wakipokea fomu za ushiriki wa shindano la Maisha Plus kutoka kwa mwanawavuti Jack Monroe. 
Kutana na Francis Bonda, mojawapo wa waandaaji na wasimamizi wa Mashindano ya Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.
Kutana na Jack Monroe, mwanawavuti wa masuala yanayohusu chakula wa www.agirlcalledjack.comkutoka nchini Uingereza. Jack ambaye yuko nchini kwa mwaliko kutoka Oxfam in Tanzania atapata fursa ya kutembelea pamoja na kuandika kuhusu mafanikio pamoja na changamoto wanazokutana nazo wakulima kutoka Tanzania. Akiwa nchini, Jack atakutana na wanachama wa kikundi cha wakulima wa mpunga Ngaya mkoani Shinyanga pamoja na kukutana na washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula waliopita.

Kutana na Mkamiti Mgawe, Afisa wa utetezi na ushawishi kutoka Oxfam. Mkamiti ametoa wito kwa wakina mama wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wakazi wa Tanzania, kuchukua fomu na kushiriki mashindano haya. Fomu za ushiriki zinaweza kujazwa moja kwa moja kupitia link hii --> http://maishaplus.tv/MamaShujaaFomu2014.html

CHANZO: Growtanzania Facebook Page


Tuesday, January 7, 2014

ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WANNE KWA MKUPUO MBEYA APOKEA MISAADA TOKA KWA WASAMARIA WEMA

Tuesday, January 7, 2014 - by Unknown · - 0 Comments


Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwasilisha msaada wa pesa na nguo toka kwa wasamaria wema akina Yassin Kapuya , Hassan Othmani, Mwandishi mwenzetu Othman Michuzi , Pendo Fundisha 





Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mpigo akiwashukuru wote waliomsaidia na wanaondelea kumsaidia kwa misaada mbalimbali kwa ajili ya watoto wake hao asema hana cha kuwalipa mungu mwenyewe ndiyo atawalipa asanteni sana

Baadhi ya waandishi wa habari waliomtembelea mama huyo na kuwasilisha michango toka wa wadau mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja

Namba ya simu ya mama huyo tutaitoa kesho kwani sasa tunamshugulikia kupata namba yake ya simu maana hana kitambulisho chochote tunawasiliana na kijiji alikotoka watupatie barua ya kupeleaka katika makampuni ya simu asajiriwe
Na Mbeya Yetu

Wednesday, January 1, 2014

HERI YA MWAKA MPYA 2014!

Wednesday, January 1, 2014 - by Unknown · - 0 Comments


A Year Of Happiness And Success!

Tunawashukuru sana kwa ushirikiano wenu wa hali na mali mliotuonyesha kwa kipindi chote cha mwaka 2013.Ombi letu kwa Mungu mfanikiwe zaidi ili muendelee kuwa pamoja nasi kwa mwaka mpya 2014.

Heri,baraka,afya,utajiri na kila lililo jema na liwe kwenu nyote kwa mwaka 2014.

Asanteni Sana.

<<<<<Jerusalem Film Team>>>>>






Monday, December 30, 2013

Video: DANIJA IPO MTAANI.......PATA NAKALA YAKO!

Monday, December 30, 2013 - by Unknown · - 0 Comments


JB mwenyewe na wakali wengine kibao utawapannda ndani ya filamu mpya ya DANIJA

Hakikisha unapata nakala halisi ya filamu hii nzuri sana kutoka Jerusalem Film Company.



Friday, December 27, 2013

GLOBAL PUBLISHERS YATOA MSAADA WA AMBULANCE BUPANDWA MHELA MKOANI MWANZA

Friday, December 27, 2013 - by Unknown · - 0 Comments


Gari la kubebea wagonjwa 'ambulance' lililotolewa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kwa wananchi wa Buchosa.
Muonekano wa gari hilo kwa ndani.…
Gari la kubebea wagonjwa 'ambulance' lililotolewa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kwa wananchi wa Buchosa.
Muonekano wa gari hilo kwa ndani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd wachapishaji wa magazeti ya Championi, Risasi, Ijumaa, Amani, Uwazi na Ijumaa Wikienda, Eric Shigongo, jana alikabidhi gari la kubebea wagonjwa 'ambulance' kwa Diwani wa Kata ya Bupandwa Mhela, Masumbuko Francis, ikiwa ni msaada kwa wakazi wa Buchosa. Pichani juu ni taswira za makabidhiano hayo yaliyofanyika jana katika sikukuu ya Krismasi huko Bupandwa Mhela, mkoani Mwanza.
(PICHA: CHANDE ABDALLAH NA DENIS MTIMA / GPL, MWANZA)

Kutoka Jerusalem Film: Hongera sana Eric Shigongo na team nzima ya GPL mmefanya jambo jema sana.Mwenyezi Mungu awabariki na awazidishie pale mlipopunguza.

CHANZO: Global Publishers

Tuesday, December 24, 2013

WAGENI WANGU............ Coming Soon!!

Tuesday, December 24, 2013 - by Unknown · - 0 Comments

Bi Staa kama anavyojulikana na wengi....

Pata uhondo kwa muhtasari......mambo kamili yaja endelea kutembelea blog yetu!!



Saturday, December 21, 2013

(Video) TANGLED MESS aka GUILTY by Cassie Kabwita!!

Saturday, December 21, 2013 - by Unknown · - 0 Comments




Baadhi ya vipande kwenye harusi ya Hemed na Cassie ( Kwenye filamu ) itakayojulikana kama Tangled Mess au Guilty.
Pata uhondo!!!

HEMED Phd AFUNGA NDOA YA SIRI NA BINTI WA KIZAMBIA!!

- by Unknown · - 0 Comments


Hemed na mkewe siku ya ndoa yao huko Lusaka Zambia


               Kuona picha zaidi za yaliyojiri siku wawili hao waliposema 'I DO' gonga HAPA.
Video fupi ya tukio hili la kufurahisha itakujia hivi punde endelea kuperuzi blog hii inayokupa habari za kipekee kabisa ambazo huwezi pata sehemu nyingine!!!!

Jisajili Kupata Habari Mpya

Ikiwa ungependa kupata taarifa zetu mara kwa mara, pindi tu zinapowekwa hapa, jisajili kwa kuandika anwani ya barua pepe hapa chini kisha fuata maelekezo

© 2013 Jerusalem Film Company. All rights reserved.
BlogTheme Edited by Rama Msangi